Psalms 10:14-17

14 aLakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,
umekubali kuyapokea mkononi mwako.
Mhanga anajisalimisha kwako,
wewe ni msaada wa yatima.
15 bVunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,
mwite atoe hesabu ya maovu yake
ambayo yasingejulikana.

16 c Bwana ni Mfalme milele na milele,
mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
17 dUnasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,
wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
Copyright information for SwhNEN